Recent Posts

HATUKUJA KUCHEZA NA ELNENY SALAH ILA MISRI ASEMA BASENA

Cairo, Misri. Baada ya kutua Misri, kocha wa timu ya taifa ya Uganda, Moses Basena amesema hawataweka akili zao zote kwa Mohamed Salah au Mohamed Elneny.
Kocha huyo wa Cranes anaamini kikosi chake kinapaswa kuwalinda vizuri wachezaji wote wa Misri katika mchezo wao wa leo usiku.
Ugandan Cranes ilishinda mchezo wake wa kwanza nyumbani kwa bao 1-0 dhidi ya vijana wa  Hector Cuper katika kusaka kwa Kombe la Dunia 2018.
“Tunakiheshimu kikosi chote cha timu ya taifa ya Misri. Hatukuja kucheza dhidi ya Mohamed Salah au Mohamed Elneny pekee,lakini tumejiandaa na kucheza na wachezaji 11 wa Misri,” alisema Basena.
HATUKUJA KUCHEZA NA ELNENY SALAH ILA MISRI ASEMA BASENA  HATUKUJA KUCHEZA NA ELNENY SALAH ILA MISRI ASEMA BASENA Reviewed by praise joe on 09:19 Rating: 5

No comments:

Theme images by i-bob. Powered by Blogger.