Recent Posts

Brazil ya kumbushia 7 za mjerumani katika Copa America leo June 9 2016 dhidi ya Haiti


Timu ya taifa ya Brazil  leo alfajiri ya June 9 2016 ilishuka dimbani kucheza mchezo wake wa pili wa michuano ya Copa America dhid ya timu ya taifa ya Haiti, katika mchezo huo Brazil ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 7-1.
Brazil ambao walikuwa na wachezaji wao nyota kasoro Neymar Junior, walianza kupata goli la kwanza kupitia kwa Philipo Coutinho aliyefunga magoli matatu yaani hat-trick kuanzia dakika ya 14, 29 na 90, Renato Agusto aliyefunga magoli mawili dakika ya 35 na 86, Gabriel dakika ya 59 na Lucas Lima dakika ya 57, wakati goli pekee la Haiti lilifungwa na James Marcelin dakika ya 70.
Kwa matokeo hayo Brazil wanakuwa wanaongoza katika msimamo wa Kundi B kwa jumla ya point 4 wakifuatiwa na Peru wenye point moja, hiyo inatokana na wao kutoa sare mchezo wa kwanza dhidi ya Ecuador, ushindi wa 7-1 kwa Brazil unajaribu kufuta machozi kwa upande wao, kwani walishawahi kufungwa goli 7-1 na timu ya taifa ya Ujerumani tena katika ardhi yao ya Brazil wakati wa michuano ya Kombe la dunia.
Brazil ya kumbushia 7 za mjerumani katika Copa America leo June 9 2016 dhidi ya Haiti Brazil ya kumbushia 7 za mjerumani katika Copa America leo June 9 2016 dhidi ya Haiti Reviewed by praise joe on 22:42 Rating: 5

No comments:

Theme images by i-bob. Powered by Blogger.