Recent Posts

Hivi kweli Trafiki wameruhusiwa kukamata makosa 10 kila siku?


Wiki hii kumekuwa na taarifa ambayo iliandikwa na baadhi ya vyombo vya habari kuwa askari wa usalama barabarani anatakiwa kukamata makosa yasiyopungua kumi kwa siku, leo June 08 2016 kamanda wa usalama barabarani  Mohamed Mpinga amelitolea ufafanuzi jambo hilo………
>>>jeshi la polisi halijawahi kuwaelekeza askari wake kukamata kiwango cha makosa kumi  kila siku barabarani askari wameelekezwa wakamate makosa mengi iwezekanavyo kutokana na kuendelea kuwepo kwa malalamiko kutoka kwa wananchi kwamba madereva wengi barabarani hawazingatii sheria za usalama barabarani na hivyo kusababisha ajali barabarani.
>>>Jeshi la polisi haliwezi kuweka kiwango cha idadi ya kukamata makosa wakati madereva wanaendelea kufanya makosa barabarani na ajali zinaendelea kutokea, ieleweke kwamba makosa ya usalama barabarani ni uhalifu unaofanywa na madereva wanapotumia barabara ambao ni sawa na uhalifu mwingine.
itizame hapa..https://youtu.be/Ifjd7qMJn-I

Hivi kweli Trafiki wameruhusiwa kukamata makosa 10 kila siku? Hivi kweli Trafiki wameruhusiwa kukamata makosa 10 kila siku? Reviewed by praise joe on 23:13 Rating: 5

No comments:

Theme images by i-bob. Powered by Blogger.