Recent Posts

Kodi ya Kusajili Gari Kwa Kuandika Jina Lako Yaongezeka Kutoka Milioni 5 Hadi 10


Serikali imebainisha kuwa kodi ya usajili wa namba binafsi kwenye magari unategemea kupanda kutoka shilingi 5,000,000 mpaka shilingi 10,000,000 kila baada ya  miaka mitatu.

Hayo yamesemwa jana Bungeni na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango alipokuwa akiwasilisha Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka wa Fedha 2016/17.

“Napendekeza kufanya marekebisho kwenye Sheria ya Magari inayohusu kodi ya Usajili na Uhamisho wa Umiliki wa magari na kufanya ada ya usajili wa namba binafsi kupanda kutoka 5,000,000 hadi shilingi 10,000,000 kila baada ya miaka mitatu,” alisema Dkt. Mpango

Akitoa sababu ya kupandisha kodi hiyo, Dkt. Mpango amesema kuwa kodi hiyo imepanda ili kuhuisha viwango vinavyopendekezwa kulingana na thamani halisi ya fedha nchini.

Aidha, Dkt Mpango alitaja kodi nyingine zinazopanda katika sheria ya magari ni pamoja na usajili wa magari kutoka shilingi 150,000 hadi shilingi 250,000 na pikipiki kutoka shilingi 45,000 hadi shilingi 95,000.

Katika hatua hiyo, Dkt. Mpango amesisitiza kuwa ongezeko hilo la kodi katika Sheria hiyo inayohusisha magari na pikipiki utaongeza mapato ya Serikali kwa kiasi cha shilingi milioni 26,915.9.

Bajeti ya Kuu ya Serikali ya mwaka 2016/17 yenye jumla ya Shilingi Trilioni 29.5 imewasilishwa Juni 8, 2016 inategemewa kujadiliwa kwa muda wa siku saba na Wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuanzia Juni 10, hadi 20, 2016 ambapo mjadala utahitimishwa kwa kura ya wazi itakayopigwa na Wabunge..
Kodi ya Kusajili Gari Kwa Kuandika Jina Lako Yaongezeka Kutoka Milioni 5 Hadi 10 Kodi ya Kusajili Gari Kwa Kuandika Jina Lako Yaongezeka Kutoka Milioni 5 Hadi 10 Reviewed by praise joe on 00:31 Rating: 5

No comments:

Theme images by i-bob. Powered by Blogger.