Recent Posts

Naibu spika kuhusu Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ kuonyesha alama ya dole bungeni


June 10 2017 naibu spika  Dr. Tulia Ackson alitangaza bungeni kuiagiza kamati ya haki, maadili na madaraka ya bunge kufanya uchunguzi wa kitendi cha Mbunge wa Mbeya mjiniJoseph Mbilinyi ’Sugu’ kudaiwa kuonyesha  kidole cha kati bungeni kitendo kinachoashiria matusi.
Naibu spika Dr. Tulia amesema…>>>’kitendo hicho kilifanyika wakati Joseph Mbilinyi alipokuwa akitoka ukumbini baada ya kuwasilisha maoni ya kambi rasmi ya upinzani kuhusu azimio la bunge kuridhia mkataba wa kimataifa wa udhibiti wa dawa na mbinu za kuongeza nguvu michezoni 
Jambo linaloombewa mwongozo linahusu maadili ya bunge, mwongozo huo unatokana kitendo cha mbunge kuonyesha kitendo chenye tafsiri ya matusi 
Kutokana na maelezo hayo na masharti ya kanuni, naelekeza kamati ya haki, maadili na madaraka ya bunge ifanye uchunguzi kuhusu kitendo kinachodaiwa kufanywa na mheshimiwa Joseph Mbilinyi na kuchukua hatua stahiki‘ – Naibu spika Dr. Tulia
Naibu spika kuhusu Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ kuonyesha alama ya dole bungeni Naibu spika kuhusu Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ kuonyesha alama ya dole bungeni Reviewed by praise joe on 02:42 Rating: 5

No comments:

Theme images by i-bob. Powered by Blogger.