Recent Posts

Zlatan Ibrahimovic amegoma kuthibitisha kama atajiunga na Man United


Mshambuliaji wa kimataifa wa Sweden ambaye alikuwa anichezea klabu ya Paris Saint Germain ya Ufaransa Zlatan Ibrahimovic, amegoma kuweka wazi kama atajiunga kweli na klabu ya Man United kama inavyoripotiwa au la, Zlatan amejibu hivyo baada ya kuulizwa swali wakati wa uzinduzi wa Clothing line yake.
Wengi walikuwa wanasubiri kwa hamu kuwa staa huyo Jumanne ya June 7 2016 atatangaza klabu gani atajiunga nayo, hiyo inatokana na Jumatatu ya June 6 kutangaza kuwa watu wakae tayari kwani Jumanne atatangaza jambo kubwa na muhimu.
zlatan-ibrahimovic-jose-mourinho-inter-milan-july-2009_3417699
Zlatan na Jose Mourinho wakati wakiwa Inter Milan pamoja
Zlatan hakutangaza kama wengi walivyotarajia kuwa hiyo ndio itakuwa siku atakayotangaza kujiunga na Man United, haikuwa hivyo kwani alitangaza kuzindua brand yake ya mavazi ya A-Z, wakati wa uzinduzi huo aliulizwa kuhusu timu gani atajiunga nayo.
Kwa sasa malengo yangu ni A-Z na haijathibitika nitajiunga klabu gani, napenda hizi stori ziendelee ili siku nikichoka nitawaambia najiunga na klabu gani, ila kwa sasa kuwa mvumilivu siwezi kusema ndio au hapana kuhusu mpango wa Man United ila malengo yangu ni A-Z, kwani hata nikiwa Man United nitavaa nguo za A-Z”
Zlatan Ibrahimovic amegoma kuthibitisha kama atajiunga na Man United Zlatan Ibrahimovic amegoma kuthibitisha kama atajiunga na Man United Reviewed by praise joe on 22:33 Rating: 5

No comments:

Theme images by i-bob. Powered by Blogger.