Uongozi Mpya Wa Yanga Watangazwa Baada Ya Kura Zote Kuhesabiwa.......Mwenyekiti ni Yusuf Manji, Makamu wake ni Clement Sanga
Yusuf Manji ameshinda nafasi ya uenyekiti wa Yanga kiulaini kutokana na kutokuwa na mpinzani kwenye nafasi hiyo hivyo kupita bila kupingwa kwenye nafasi ambayo alikuwa akiitetea.
Clemen Sanga nae amepenya katika nafasi ya Makamu Mwenyekiti kwa kumbwaga mpinzani wake Titus Osoro.
Shughuli pevu ilikuwa kwa wagombea nafasi ya ujumbe ambapo jumla ya wagombea 20 walikuwa wakiwania nafasi 8 za ujumbe.
Mwenyekiti
Yusuf Manji ameibuka mshindi wa nafasi ya uenyekiti akipenya bila kupingwa na kupata idadi ya kura 1468 zilizopigwa na wanachama, huku kura 2 pekee zikiwa zimeharibika.
Makamu Mwenyekiti
Clement Sanga amemgaragaza mpinzani wake baada ya kupata kura 1428 wakati mpinzani wake Titus Osoro akiambulia kura 80 pekee.
Wajumbe
Ayoub Nyenzi (889), Salim Mkemi (894), Bakar Malima (577), Godfrey Mheluka (430), David Ruhago (582), Lameck Nyambaya (655), Sylvester Haule (197), Pascal Laizer (178), Samwel Lukumay (818), Hashim Abdallah (727), George Manyama (249), Hussein Nyika (770), Siza Lyimo (1027), Beda Tindwa (452),Tobias Lingalangala (889), Athumani Kihamia (558), Mchafu Chakoma (69), Edgar W Chibura (72), Ramadhani M. Kampira (182), Omary S. Amei (1069)
Kwa Matokeo hayo, uongozi mpya wa Yanga uliochaguliwa na wanachama unaundwa na Mwenyekiti Yusuf Manji, Makamu Mwenyekiti Clement Sanga huku wajumbe wakiwa ni Omary S. Amei, Siza Lyimo, Salim Mkemi, Tobias Lingalangala, Ayoub Nyenzi, Samwel Lukumay, Hussein Nyika na Hashim Abdallah
Uongozi Mpya Wa Yanga Watangazwa Baada Ya Kura Zote Kuhesabiwa.......Mwenyekiti ni Yusuf Manji, Makamu wake ni Clement Sanga
Reviewed by praise joe
on
00:54
Rating:
No comments: