Recent Posts

Mchezaji tennis Maria Sharapova amefungiwa miaka miwili kucheza mchezo huo


Ukizungumzia wanamichezo wanawake matajiri duniani huwezi kuacha kulitaja jina laMaria Sharapova ambaye ni mcheza tennis maarufu. Maria Sharapova ameingia kwenye headlines baada ya kuripotiwa kufungiwa kucheza Tennis kwa muda wa miaka miwili, hiyo ni baada ya vipimo kuthibitisha kuwa anatumia madawa ya kusisimua misuli.
sharapooShirikisho la Tennis la kimataifa duniani (ITF) limemfungia Maria Sharapova baada ya kugundua kuwa amekuwa akitumia dawa hizo za kusisimua misuli aina ya Meldonium kwa muda mrefu.
Shirikisho hilo limetangaza rasmi June 8 2016 kuwa mrembo huyo hatoruhusiwa kucheza tennis kwani amekiuka sheria za michezo, ingawa imetangazwa rasmi kufungiwa kwake, Maria Sharapova anasema yeye amekuwa akitumia  dawa hizo kwa  matibabu ya moyo tangu mwaka 2006.
Mchezaji tennis Maria Sharapova amefungiwa miaka miwili kucheza mchezo huo Mchezaji tennis Maria Sharapova amefungiwa miaka miwili kucheza mchezo huo Reviewed by praise joe on 23:52 Rating: 5

No comments:

Theme images by i-bob. Powered by Blogger.