Winga wa Azam, Joseph Kimwaga, atakaa nje ya uwanja miezi minne baada ya kubainika kuwa amechanika mtulinga wa kati ‘meniscus’ kwenye goti lake la mguu wa kushoto.
Kimwaga tangu Ijumaa iliyopita yuko nchini Afrika Kusini alikoenda kwa matibabu ya goti lake hilo, aliloumia wakati Azam ikijiandaa na mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Ndanda wiki mbili zilizopita.
Mchezaji huyo anatarajiwa kufanyiwa upasuaji mdogo kesho Alhamis na atakuwa nje ya uwanja kwa miezi minne au zaidi.
Daktari wa Azam,Mwanandi Mwankemwa alisema mchezaji huyo alifanyiwa vipimo jana Jumatatu na Dr. Nickolas kwenye Hospitali ya Vincent Palloti iliyopo jijini Cape Town nchini humo.
“Jana alifanyiwa vipimo na kuthibitika amechanika Meniscus upande wa kati"alisema Mwankemwa baada ya kupokea ripoti kutoka kwa Dr. Nickolas.
Aliongeza"Baada ya kufanyiwa kipimo hicho, Kimwaga atalazwa kesho(leo) na Alhamis atafanyiwa upasuaji mdogo (athroscopy) na Jumamosi atatoka Hospitali na anatarajiwa kurejea Tanzania Septemba 13.
Mwankemwa alisema upasuaji wa kwa njia ya Athroscopy ni ule wa kisasa kabisa ambao wataalamu hutumia vifaa maalum, ambavyo huingizwa kwenye goti na hufanya matibabu na kuondoa matatizo yote katika eneo hilo, faida yake humfanya mchezaji kurejea mapema uwanjani kuliko ule wa kupasuliwa goti zima.
WINGA WA AZAM FC , KIMWAGA,KUKAA NJE MIEZI MINNE
Reviewed by praise joe
on
09:02
Rating:
No comments: